Imearifiwa kuwa msomo mwandamizi wa Saudi Arabia amewasilisha mpango ambao unatafakariwa na wasimamizi wa al Masjid al-Nabawi katika mji mtakatifu wa Madina ambapo Mtume SAW amezikwa chini ya Kuba la Kijani Kibichi. Msikiti huo wa Mtume SAW hutembelea na mamilioni ya Waislamu kila mwaka na unatambuliwa kama sehemu ya pili takatifu zaidi katika Uislamu.
Kwa mujibu wa taarifa katika gazeti la Independent la Uingereza, waraka wenye kurasa 61 umependekeza kuwa mwili wa Mtume Muhammad SAW uhamishiwe katika makaburi yaliyokaribu ya al Baqi ambapo utazikwa katika sehemu isiyojulikana katika makaburi hayo ambamo pia wamezikwa Ahlul Bayt AS. Kwa mujibu wa pendekezo hilo lililowasilishwa kuba la al-Masjid al Nabawi pia litabomolewa. Pendekezo hilo limewasilishwa na Dkt. Irfan al-Alawi Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Turathi ya Kiislamu.
Dkt. al-Alawi amekiri kubwa mpango huo ukitekelezwa kutaibuka machafuko katika ulimwengu wa Kiislamu