IQNA- Ustadh Hadi Mowahhed Amin, qari wa kimataifa wa Iran, asubuhi ya Mosi Shawwal 1446 Hijria (31 Machi 2025) katika mwanzo wa hafla ya Swala ya Idul Fitr jijini Tehran, alisoma aya za Surah ya Al-A‘laa katika Qur'ani Tukufu. Swala hiyo iliswalishwa na Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.
Habari ID: 3480494 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/04/04
Wapalestina karibu laki moja wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr Alkhamisi asubuhi katika Msikiti wa al Aqsa ambao ni Kibla cha Kwanza cha Waislamu katika mji wa Quds (Jerusalem) licha ya sheria kali zilizowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel ambao siku chache zilizopita wanajeshi wa utawala huo katili waliwashambulia kwa mabomu Waislamu waliokuwa wanasali ndani ya Msikiti huo.
Habari ID: 3473911 Tarehe ya kuchapishwa : 2021/05/15