iqna

IQNA

nairuzi
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa munasaba wa Nowruz
TEHRAN (IQNA)-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei, ametuma ujumbe kwa mnasaba wa Nowruz (Nairuzi) ambayo ni siku kuanza mwaka mpya wa 1402 Hijria Shamsia ambapo ametoa pongezi kwa wananchi wa Iran na mataifa yote yanayosherehekea Nowruz.
Habari ID: 3476735    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/21

Ustaarabu
TEHRAN (IQNA)- Mwaka mpya wa Kiirani Hijria Shamsia wa 1402 unaanza 21 Machi 2023 Miladia. Siku za kuanza mwaka mpya wa Kiirani hujulikana kama Nowruz au Nairuzi kwa lugha ya Kiswahili na huadhimishwa kwa furaha na shangwe kote Iran na nchi zinazozungumza Kifarsi pamoja na mataifa yote ambayo kwa njia moja au nyingine yana uhusiano na ustaarabu na utamaduni wa Iran.
Habari ID: 3476733    Tarehe ya kuchapishwa : 2023/03/20

TEHRAN (IQNA)-Katika ujumbe wake kwa mnasaba wa kuanza mwaka 1401 Hijria Shamsia, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amelipongeza taifa kwa kuwadia sikukuu ya Nowruz au Nairuzina kuutaja mwaka mpya kuwa ni mwaka wa "uzalishaji unaotegemea elimu na kutengeneza ajira."
Habari ID: 3475062    Tarehe ya kuchapishwa : 2022/03/21

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wa Nairuzi*
TEHRAN (IQNA) - Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja mwaka mpya wa Kiirani wa 1399 Hijria Shamsia ulioanza leo nchini Iran kuwa ni Mwaka wa Ustawi Mkubwa katika Uzalishaji na kusema: Hatua kubwa ya uzalishaji inapaswa kuleta mabadiliko yanayohisika katika maisha ya wananchi.
Habari ID: 3472584    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/20

Rais Hassan Rouhani katika ujumbe wa Nairuzi*
TEHRAN (IQNA)- Rais Hassan Rouhani wa Iran ametuma ujumbe wa munasaba wa mwaka mpya wa Kiirani wa 1399 Hijria Shamsiya na kusema mwaka mpya utakuwa mwaka wa afya, ajira na ustawi wa kiuchumi na kiutamaduni nchini Iran.
Habari ID: 3472583    Tarehe ya kuchapishwa : 2020/03/20

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe wa kuanza mwaka mpya wa 1395 Hijria Shamsia akiwapa mkono wa kheri ya mwaka mpya na Nairuzi wananchi wote na Wairani hususan familia tukufu za mashahidi na majeruhi wa vita.
Habari ID: 3470206    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/20

Tarehe 20 au 21 Machi husadifiana na tarehe Mosi Farvardin, siku ya kuanza mwaka mpya wa Kiirani wa Hijria Shamsia, siku ambayo ni maarufu kama Nowruz au kwa Kiswahili Nairuzi. Kuwadia kwa mwaka mpya wa Hijria Shamsia ambao aghalabu huadhimishwa Iran huenda sambamba na kuingia msimu wa machipuo na mabadiliko katika miti, mimea maua na majani.
Habari ID: 3470204    Tarehe ya kuchapishwa : 2016/03/18

Ujumbe wa Nairuzi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
Ayatullah Udhma Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa ujumbe maalumu kwa wananchi wa Iran kwa mnasaba wa kuingia mwaka mpya wa 1393 Hijria Shamsia na kuuita mwaka huo kwa jina la mwaka wa "Uchumi na Utamaduni wenye Azma ya Kitaifa na Uongozi wa Kijihadi."
Habari ID: 1389135    Tarehe ya kuchapishwa : 2014/03/21