IQNA

Maonyesho ya kimataifa ya Qur'ani yaanza Tehran

20:02 - June 25, 2014
Habari ID: 1422668
Maonyesho ya 22 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yamefungua milango yake kwa watazamaji leo Jumatano hapa mjini Tehran.

Maonyesho hayo ambayo yamefunguliwa rasmi na Ali Jannati, Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran yanafanyika katika uwanja wa Bustani ya Kujihami Kutakatifu  ambapo taasisi 53 zinazoshiriki katika maonyesho hayo.
Maonyesho hayo yanatazamiwa kuendelea hadi katikati ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na yanafunguliwa kila siku kuanzia saa moja usiku hadi saa sita usiku.
Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho hayo Waziri wa Utamaduni na Muongozo wa Kiislamu wa Iran Ali Jannati amesema maonyesho hayo yanafanyika kwa lengo la kuhimiza na kueneza utamaduni na Qur'ani na mtindo wa maisha kwa mujibu wa mafundisho ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.

1422175

Kishikizo: Qur ani, maonyesho, tehran
captcha