Maonyesho hayo ya Qur'ani ambayo yanafanyika kuadhimisha mwaka 1404 tangu kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu kiteremshwe, yalifunguliwa na kiongozi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Congo na mabalozi wa nchi za Kiislamu katika ukumbi wa al Kauthar.
Maonyesho hayo pia yana nakala mbalimbali za chapa ya Qur'ani Tukufu kwa lugha tofauti za Kiafrika na baadhi ya zana zinazonasibishwa kwa Mtume Muhammad (saw) kama mavazi yake. Maonyesho hayo yataendelea hadi tarehe 25 Julai.
Baadhi ya watu waliotembelea maonyesho hayo pia wametunukiwa zawadi za tarjumi ya Qur'ani Tukufu.
1426210