IQNA

Makumbusho ya Maisha ya Mtume Muhammad (SAW) na Ustaarabu wa Kiislamu Yazinduliwa Makkah

11:14 - August 29, 2025
Habari ID: 3481152
IQNA – Maonyesho ya Kimataifa na Makumbusho ya Maisha ya Mtume Muhammad (SAW) pamoja na Ustaarabu wa Kiislamu yamezinduliwa katika Mnara wa Saa, katika mji mtukufu wa Makkah, siku ya Jumanne.

Naibu Gavana wa Mkoa wa Makkah, Mwanamfalme Saud bin Mishaal bin Abdulaziz, ndiye aliyefungua rasmi makumbusho hayo na maonyesho hayo.

Maonyesho haya yameandaliwa chini ya usimamizi wa Jumuiya ya Kiislamu ya Dunia (MWL) kwa ushirikiano na Tume ya Kifalme ya Mji wa Makkah na Maeneo Matakatifu, yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali.

Bin Mishaal bin Abdulaziz alitembelea mabanda na maonyesho mbalimbali yanayowapa wageni fursa ya kujifunza kwa kina na kushiriki kwa njia ya kisasa kuhusu maisha ya Mtume Muhammad (SAW) na ustaarabu wa Kiislamu, kwa kutumia teknolojia za kisasa za kuona na kidijitali.

Miongoni mwa vivutio vya tukio hilo ni banda la “Mtume Kama Ungelikuwa Pamoja Naye,” linaloonyesha mandhari ya Makkah, Madinah, na njia ya Hijrah, pamoja na maonyesho ya chumba cha Mtume, banda la tiba ya Mtume, na uwasilishaji wa ratiba ya kila siku ya maisha Mtume, katika safari ya kiroho inayowazamisha wageni katika mazingira ya maisha ya Mtume Muhammad (SAW) kama vile wanayashuhudia kwa macho.

Mwanamfalme Saud bin Mishaal bin Abdulaziz pia alielezewa kuhusu jukwaa la kidijitali linaloambatana na tukio hilo, ambalo linajumuisha maktaba ya kielimu na ensaiklopidia za maarifa zilizotafsiriwa kwa lugha muhimu duniani, likiwa ni njia ya kisasa ya kusambaza historia na Sira ya Mtume Muhammad (SAW).

 3494400

captcha