IQNA

Maonyesho ya Makka yamulika historia ya Kaaba

18:23 - March 10, 2025
Habari ID: 3480343
IQNA – Masjid al Haram au Msikiti Mkuu katika mji mtukufu wa Makka ni mwenyeji wa maonyesho kuhusu historia ya Kaaba.

Maonyesho haya yanayojulikana kama "Nyumba ya Kwanza", yanawasilishwa katika lugha 10 na yanaeleza historia ya ujenzi wa Kaaba katika vipindi tofauti vya historia, kuanzia wakati wa Nabii Ibrahim (AS) hadi sasa.

Waislamu kote duniani huelekea Kaaba wanaposwali.

Maonyesho haya, yanayofanyika katika sehemu ya upanuzi wa Msikiti Mkuu, yanawapa wageni na mahujaji fursa ya kipekee ya kufuatilia hatua za ujenzi wa Kaaba kupitia maonyesho ya picha, michoro, vitu vya kihistoria, na skrini shirikishi.

Maonyesho haya yameandaliwa na Mamlaka Kuu ya Uangalizi wa Misikiti Miwili Mitukufu wakati wa Ramadhani, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwatambulisha Waislamu historia ya Msikiti Mkuu na maeneo yake muhimu kwa kutumia teknolojia za kisasa za mawasiliano.

Mada kuu za maonyesho haya zinajikita katika:

  • Ujenzi wa Kaaba Mabadiliko ambayo imepitia katika historia Vifaa vilivyotumiwa katika kuitunza na kuiosha Hatua za utengenezaji wa sitara yake au pazia (Kiswah)

Ramadhani kwa kawaida huwa ni msimu wa kilele wa Umrah, au hija ndogo, katika Msikiti Mkuu, huku mamlaka zikijiandaa kikamilifu kukabiliana na wingi wa waumini.

Msimu wa sasa wa Umrah, ambao unaweza kufanywa mwaka mzima, ulianza mwishoni mwa Juni baada ya kumalizika kwa Hija ya kila mwaka.

3492251

Kishikizo: makka maonyesho kaaba
captcha