IQNA

Maonyesho ya Muharram nchini Tanzania yazingatia subira ya Bibi Zaynab (SA)

16:03 - July 22, 2025
Habari ID: 3480984
IQNA – Mwaka huu, kwa mara ya sita mfululizo, vijana Waislamu wa madhehebu Kishia wa jamii ya Khoja Ithnashari nchini Tanzania wameandaa maonyesho ya Muharram yenye kaulimbiu ya "Subira na Msimamo wa Bibi Zaynab (SA)”.

Kwa mujibu wa Kituo cha Kitamaduni cha Iran nchini Tanzania, maonyesho ya mwaka huu yamejikita katika ustahimilivu wa Bibi Zaynab (SA), mwanamke mashuhuri aliyeisimulia harakati ya Ashura na akawa alama ya subira, ujasiri, na hekima.

Maonyesho haya yana sehemu mbalimbali zenye mchanganyiko wa sanaa ya maonyesho na athari za kuona, zikiwemo taswira za masaibu ya bibi huyu mkubwa huko Karbala na baada ya hapo. Pia kuna uwasilishaji wa matukio ya Karbala, ikulu ya Yazid, na soko la Damascus, pamoja na eneo la tafakari na kutulia kiroho.

Katika sehemu ya mwisho ya maonyesho hayo, kuna nakala za kisanaa na zenye kuvutia za kaburi takatifu la Bibi Zaynab (SA), eneo la Bain-ul-Haramain (kati ya Haram ya Imam Hussein (AS) na Abbas (AS) huko Karbala), na kaburi la Imam Hussein (AS).

Mohsen Maarefi, mwambata wa utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania, alitembelea maonyesho hayo na kuyasifu kuwa ni juhudi za kisanii, zenye dhamira, na zenye kugusa nyoyo.

Alisifu sana mpangilio mzuri wa maonyesho hayo na uchaguzi wa busara wa mada, akisema:

"Katika dunia ya leo ambapo vyombo vya habari na simulizi vinaathiri sana mitazamo ya jamii, tunahitaji zaidi ya wakati wowote kuiga mfano wa Bibi Zaynab (SA), mwanamke aliyepeleka ujumbe wa Ashura hadi masikioni mwa dunia, na hakuruhusu watawala waongo kupotosha ukweli au kufanikisha malengo yao maovu.”

Maonyesho hayo yalizinduliwa rasmi siku ya Alhamisi 17 Julai, na yalimalizika Julai 21, 2025.

.

 
 

3493922

captcha