IQNA

Jina ‘Muhammad’ laongoza Orodha ya Majina Maarufu ya Watoto Wavulana nchini Uingereza

21:41 - December 06, 2024
Habari ID: 3479867
IQNA - Kulingana na data ya hivi punde kutoka Ofisi ya Takwimu ya Kitaifa Uingereza (ONS), Muhammad limekuwa jina la mtoto maarufu zaidi la wavulana England na Wales mnamo 2023.

Takwimu hizo zinaashiria mabadiliko makubwa, kwani jina hilo limekuwa katika 10 bora tangu 2016 na lilikuwa la pili kwa umaarufu mnamo 2022, gazeti la Express liliripoti Alhamisi.

Jina la Mtume wa Uislamu, Muhammad (SAW), ambalo kwa Kiarabu linamaanisha " Mwenye kusifiwa," sasa limepita jina la ‘Noah’ ambalo lilishika nafasi ya kwanza mnamo 2021 na 2022.

ONS hukusanya data hii kulingana na waliosajiliwa  pindi baada ya kuzaliwa  England na Wales.

Wakati Muhammad lilikuwa jina linaloongoza katika mikoa minne kati ya tisa ya England, lilishika nafasi ya 63 nchini Wales. Kwa jumla, watoto 4,661 waliitwa Muhammad kote England na Wales, ikilinganishwa na 4,382 walioitwa Noah.

Takwimu pia zinaonyesha kuwa Muhammad alikuwa maarufu sana miongoni mwa akina mama wenye umri wa miaka 25 na zaidi.

Jina hili lina tahajia mbalimbali, na kama hizi zingeunganishwa katika miaka iliyopita, jina ‘Muhammad’ lingeshika nafasi ya kwanza mapema.

Licha ya tahajia tofauti, umaarufu wa jumla wa jina hilo unaongezeka katika jamii mbali mbali. 

3490948

Kishikizo: Mohammad jina uingereza
captcha