Muhammad Abdur Rahman amedai kuwa muujiza wa kisayansi wa Qur'ani ni aina fulani ya kudhalilisha Qur'ani. Amesema kuwa hatua ya Waziri wa Elimu wa Misri ya kuruhusu somo la muujiza wa kisayansi wa Qur'ani ni upuuzi mtupu.
Mtangazaji huyo amehoji akisema kazi hiyo isiyo na faida inafundishwa vipi kwa watoto wa Misri!
Ripoti zinasema kuwa Waziri wa Elimu wa Misri Mahmoud Abu Nasr amekutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Muujiza wa Kisayansi wa Qur'ani mjini Cairo na kutoa habari ya kuanza kutayarishwa mtaala wa kufundisha muujiza wa kisayansi wa Qur'ani n Suna katika shule za nchi hiyo.
Kabla ya hapo pia chama cha kilaiki cha Misri kilipinga vikali pendekezo la Wizara ya Elimu la kufundishwa muujiza wa kisayansi wa Qur'ani katika shule za Misri.