IQNA

Waislamu Marekani watangaza amani na suluhu

20:04 - October 14, 2014
Habari ID: 1460244
Kundi la Waislamu wa mji wa Buffalo katika jimbo la New York huko Marekani imewagawia wananchi wa mji huo mashada ya maua yenye semi na maneno ya Mitume wa dini za mbinguni.

Mjumbe wa kundi Jumuiya ya Waislamu wa Buffalo (WNY) Samad Khan amesema lengo la hatua hiyo ni kuhubiri utamaduni wa mazungumzo baina ya dini tofauti na kuanzisha anga ya kukutana pamoja wafuasi wa dini hizo kwa kutumia maua.
Amesema kutoa zawadi ya ua ni kazi ndogo lakini ni nembo ya kimataifa ya upendo na mfungamano.
Samad Khan amesema kuwa dini za Ukristo, Uyahudi na Uislamu pia zinasisitiza juu ya udharura wa kueneza upendo, mshikamano na amani.
Hatua hiyo ya kundi la Waislamu wa mji wa Buffalo imepongezwa sana na wananchi wa Marekani. Hii ni mara ya pili kwa Waislamu wa mji huo kuchukua hatua kama hiyo ambayo miongoni mwa malengo yake ni kuonesha upinzani wa dini ya Uislamu dhidi ya jinai na ukatili unaofanywa na kundi la kigaidi la Daesh. AIR 1459926

captcha