IQNA

Makundi ya Kiislamu yanapaswa kuungana katika kumtetea Mtume

14:18 - November 06, 2008
Habari ID: 1705166
Mufti wa Misri Ali Juma ameyataka makundi ya Kiislamu kuunganisha pamoja juhudi zao kwa ajili ya kumtetea Mtume Muhammad SAW.
Gazeti la al Watan la Saudi Arabia limemnukuu Mufti wa Misri akisema kuwa jumuiya, mashirika na makundi yote ya Kiislamu katika nchi za Kiarabu na Kiislamu yanapaswa kuungana kwa ajili ya kumtetea Mtume Muhammad SAW.
Mufti Juma amesisitiza juu ya udharura wa kuainishwa taratibu maalumu za kukabiliana na vitendo vya kuzivunjia heshima dini, Mitume wa Mwenyezi Mungu, itikadi na matukufu ya kaumu mbalimbali na akasema kuwa, Waislamu wanapaswa kuweka kando hitilafu zao za kimadhehebu na kutumia suhula zao kwa ajili ya kuitetea dini hiyo na matukufu yake.
Mufti wa Misri ameashiria mikutano iliyofanyika hadi sasa kwa ajili ya kumtetea Mtume Muhammad mbele ya hujuma za maadui wa Uislamu na akasema kuwa mikutano hiyo imefanyika kujadili mipango na mapendekezo ya jinsi ya kumtetea kivitendo Mtume wa Mwenyezi Mungu SAW.
Sheikh Ali Juma amesema kuwa malengo mengine ya mikutano hiyo ni kuchunguza mipango ya baadaye hususan ya kumtetea Mtume wa Mwenyezi Mungu katika jamii zisizokuwa za Kiislamu. 316196
captcha