Syria imechaguliwa kuwa sehemu ya kufanyika kikao hicho cha siku tatu kutokana na kuchaguliwa kwake kuwa kituo cha utamaduni cha nchi za Kiarabu. Wanafikra na wasomi mbalimbali wa nchi za Kiarabu na Kiislamu watashiriki katika kikao hicho na kuwasilisha makala pamoja na hotuba mbalimbali za kuimarisha umoja na kushajiisha kufanyika mazungumzo na vilevile kuimarishwa shughuli za utamaduni za nchi za Kiislamu. Mshikamano wa kiutamaduni katika zama za utandawazi, changamoto, mfungamano wa Kiislamu katika kulinda jamii za wachache za Waislamu na kuwashirikisha katika juhudi za kutoa sura halisi ya Uislamu katika jamii wanazoishi, ni miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa na kujadiliwa katika kikao hicho. 317611