Kitabu cha Hamasa, Hadhi ya Mashujaa" ambacho kinazungumzia maudhui ya mapambano ya wananchi shujaa wa Palestina dhidi ya ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel, kimezinduliwa katika Kituo cha Fasihi cha Moscow nchini Russia.
Kitabu hicho kimeandikwa na mwandishi mashuhuri wa Russia Alexander Bryukhanov.
Katika kitabu hicho, Bryukhanov ameandika makala kuhusu mapambano ya kujitetea ya wananchi wa Palestina, ushirikiano zaidi wa Russia na ulimwengu wa Kiislamu na lawama na malalamiko yake dhidi ya uchapishwaji wa picha zinazomvunjia heshima Mtume Muhamma SAW.
Sherehe za uzinduzi wa kitabu hicho zimehudhuriwa na Usama Hamdan ambaye ni mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya harakati ya Hamas, mabalozi kadhaa wa nchi za Kiarabu na wataalamu wa fasihi, masuala ya kijamii na Kiislamu wa Russia.
Mwandishi huyo mashuhuri wa Russia amesema katika sherehe za uzinduzi wa kitabu hicho kwamba, mapambano ya wananchi shujaa wa Palestina dhidi ya wavamizi wanaoikalia Quds kwa mabavu yanamkumbusha mapambano ya mashujaa wa Russia dhidi ya uvamizi wa Wajerumani nchini humo katika Vita vya Pili vya Dunia.
Amesema, anatarajia kukutana na wakazi wa Palestina katika siku za usoni katika mji mkuu wa taifa la Palestina wa Quds Tukufu. 322244