IQNA

12:43 - November 20, 2008
Habari ID: 1710461

Mufti Mkuu wa Bosnia akutana na balozi wa Uingereza

Mufti Mkuu wa Bosnia Herzegovina Sheikh Mostafa Afendi Tasrich amekutana na Michael Titian Balozi wa Uingereza mjini Sarajevo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA katika eneo la Balkan, Sheikh Mostanfa Afendi amelezea kuridhishwa kwake na balozi aliyeondoka wa Uingereza mjini Sarajevo na kuelezea matumaini yake kuwa jamii ya Waislamu itakuwa na ushirikiano mzuri na Ubalozi wa Uingereza.
Naye Michael Titian amepongeza nafasi ya jamii ya Waisalmu Bosnia katika kurejesha amani nchini humo. Amesisitiza juu ya umuhimu wa watu kuishi pamoja kwa amani na kuvumiliana nchini na kusema, hilo litatoa mchango mkubwa na umuhimu katika shughuli za Mufti wa Bosnia Herzegovina katika kuimarisha mazungmzo baina ya dini duniani. 322564
captcha