IQNA – Zaidi ya watu 10,000 wametembelea Kituo cha Uchapishaji wa Qur’an Tukufu cha Mfalme Fahd kilichopo Madina wiki iliyopita.
Kituo hicho cha uchapishaji kimefikia idadi ya juu kabisa ya wageni kwa siku moja katika historia yake Alhamisi iliyopita, kikipokea wageni 10,558 kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Hii inadhihirisha juhudi endelevu katika kuhudumia Qur’an Tukufu na Waislamu ulimwenguni kote.
Katika ziara yao kwenye kituo hicho, wageni walijionea machapisho mbalimbali ya Qur’an Tukufu pamoja na tafsiri za maana zake katika lugha zaidi ya 80.
Walijifunza kuhusu juhudi za kituo hicho katika kuchapa, kuchapisha, na kusambaza maana na mwongozo wa Qur’an Tukufu kwa Waislamu katika lugha zao husika.
Idadi hii kubwa ya watembeleaji inasisitiza azma ya kituo hicho katika kuhifadhi Qur’an Tukufu, kudumisha machapisho yake, na kuwapa wageni uzoefu bora wa kielimu, sanjari na dhamira yake kuu ya kuhudumia na kueneza Qur’an miongoni mwa Waislamu ulimwenguni kote.
/3498675