Majlisi ya maombolezo ya Arbaeen, ambayo mwaka huu iliangukia tarehe Agosti 4, ni miongoni mwa mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini duniani.
Arbaeen huadhimisha siku ya arobaini baada ya Ashura, kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW), Imam Hussein (AS).
Kila mwaka, umati mkubwa wa Waislamu wa Shia humiminika Karbala, ambako iko Haram Tukufu ya Imam Hussein (AS), kwa ajili ya kutekeleza ibada na taratibu za maombolezo.
Mazuwar, hasa kutoka Iraq na Iran, husafiri masafa marefu kwa miguu kuelekea mji huo mtukufu.



4367992