IQNA

Ofisi ya Rais Afghanistan yaratibu safari za Hija

11:26 - November 22, 2008
Habari ID: 1710996
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan amesema ofisi yake inaratibu kikamilifu mpango wa mahujaji ili kuhakikisha safari hiyo ya kimaanawi inafanyika kwa kiwango cha juu kabisa.
Rais Karzai ameyasema hayo katika uwanja wa ndege wa Kabul alipoenda kuwaaga Mahujaji. Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Afghanistan, Rais Karzai amewaomba radhi mahujaji wa nchi hiyo kutokana na kuvurugika safari za kuelekea Makka jambo ambalo limepelekea baadhi yao kuchelewa kufika katika mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia. Rais Karzai pia ameahidi kuwa Mahujaji wote nchini humo watafika kwa wakati nchini Saudi Arabia ili waweze kutekeleza ibada ya hija ipasavyo.
Katika siku za hivi karibuni mahujaji kadhaa wa Afghanistan hawakuweza kuanza safari zao kwa wakati ulioainishwa kutokana na matatizo yaliyosababishwa na Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano na Wizara ya Hija na Masuala ya Wakfu.
323288

captcha