IQNA

Kuendelea jinai za Marekani dhidi ya Waislamu katika jela za Afghanistan

12:26 - November 22, 2008
Habari ID: 1711054
Mwandishi mmoja wa habari Muislamu kutoka Uingereza amelaani jinai za Marekani dhidi ya Waislamu katika jela za Afghanistan na amefichua kuendelea na kukithiri vitendo vya mateso hasa dhidi ya wanawake katika jela hizo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA nchini Afghanistan, Maryam Yvonne Ridley amefichua hayo akiwa nchini Pakistan na ametaka kufanyike juhudi za kuwanusuru wanawake hao Waislamu ambao wanashikiliwa mateka na wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Afghanistan. Ameongeza kuwa wanawake 650 Waislamu Waafghani wanashikiliwa katika jela za kuogofya za Marekani ambapo wanakabiliwa na mateso makali mno.
"Kuna wanawake wengi Waislamu ambao wanashikiliwa mateka na vikosi vya Marekani, na iwapo tutanyamazia kimya jinai hizo, basi tutawapoteza dada zetu Waislamu", amesema Yvonne Ridley.
Mwanaharakati huyu Muislamu Muingereza pia amelaani vikali hatua ya wanajeshi vamizi wa Marekani kuwatia mbaroni kiholela na kinyume cha sheria raia wa Afghanistan. Ridley ametoa mwito kwa Waislamu kuungana na kusema kuwa Wamarekani wanaogopa kuona watu wa Pakistan na Afghanistan wakiungana na kuwa na mshikamano.
323276
captcha