IQNA

10:58 - November 27, 2008
Habari ID: 1713212

Tamasha la sita la mavazi ya Kiislamu laanza nchini Malaysia

Tamasha la sita la mavazi ya Kiislamu lilianza mjini Kuala Lumpur Malaysia siku ya Jumanne.

Kwa mujibu wa tovuti ya Allnewsweb, zaidi wa wataalamu wa mitindo ya mavazi ya Kiislamu 40 kutoka nchi za Indonesia, India, Pakistan na Ufilipino wanashiriki katika tamasha hilo kwa kuonyesha mitindo na mbinu zao katika ushonaji wa mavazi ya Kiislamu. Lengo la kuandaliwa tamasha hilo lemetajwa kuwa ni kuwasilisha nguo na mavazi maridadi yanayozingatia na kwenda sambamba na sheria za Kiislamu. Tamasha hilo linatazamiwa kumalizika leo Alkhamisi, ambapo maonyesho na soko la nguo za Kiislamu pia litazinduliwa kesho Ijumaa katika hoteli ya Marriot mjini Kuala Lumpur, na kuendelea kwa muda wa wiki moja. 325928
captcha