IQNA

11:48 - November 30, 2008
Habari ID: 1714102

Kikao cha pili cha viongozi wa kidini wa Afrika kufanyika Disemba

Kikao cha pili cha viongozi wa kidini wa bara la Afrika kitafanyika kati ya tarehe 3 hadi 5 za mwezi Disemba pambizoni mwa kikao cha kimataifa cha 'dini kwa ajili ya amani' barani humo.

Kwa mujibu wa tovuti ya Islamic Call, lengo kuu la kufanyika kikao hicho ambacho kitaandaliwa kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Wito wa Kiislamu na ambacho kitafanyika chini ya anwani ya 'kukabiliana na utumiaji nguvu na kuenezwa usalama katika kivuli cha ushirikiano wa dini' limetajwa kuwa ni kuenezwa amani barani Afrika. Kubuniwa kwa mfumo utakaozingatia thamani za kidini ni lengo jingine la kufanyika kikao hicho ambacho kimepangwa kufanyika katika mojawapo ya nchi za Kiafrika ambayo hadi sasa haijaainishwa. Kikao hicho kitakachohudhuriwa na viongozi 140 wa kidini barani Afrika kitachunguza migogoro ya hivi sasa barani Afrika na kutafutwa njia za kukabiliana na hatimaye kumaliza migogoro hiyo. 327306
captcha