IQNA

Maulama wa Kishia na Kisuni wa Iraq kukutana leo mjini Makka

12:50 - December 04, 2008
Habari ID: 1715791
Maulama wa Kishia na Kisuni wa Iraq wanakutana leo mjini Makka, Saudi Arabia kuchunguza umoja wa kitaifa na Kiislamu nchini humo.
Mwenyekiti wa Idara ya Waqfu ya Masuni wa Iraq Ahmad Abdulghafur al Samurai amesema kuwa kikao hicho kitahudhuriwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu (OIC) Ekmeleddin Ihsanoglu, maulama wa Kishia na Kisuni wa Iraq, wanafikra na shakhsia mbalimbali wa nchi hiyo.
Al Samurai amesema kuwa miongoni mwa ajenda za kikao hicho ni kuchunguza njia za kuimarisha umoja na mshikamano wa kitaifa na Kiislamu nchini Iraq na maazimio ya Hati ya Makka iliyopasishwa mwaka 2006 kwa shabaha ya kulinda umoja na kuharamisha umwagaji wa damu ya Waislamu.
Ahmad al Samurai amesema kuwa mkutano wa leo wa wanazuoni wa Kiislamu wa Shia na Suni mjini Makka ni utangulizi wa mkutano wa Kiislamu wa kimataifa uliopangwa kufanyika baada ya msimu wa Hija wa mwaka huu mjini Baghdad. Mkutano huo ambao utasimamiwa na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu utahudhuriwa na shakhsia wa Kiislamu na kisiasa kutoka nchi mbalimbali duniani. 329609
captcha