Stephan De Mistura, Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amewapongeza na kuwatakia sikukuu njema ya Idul Adh’ha, Waislamu na serikali ya nchi hiyo pamoja na Waislamu wote ulimwenguni.
Katika ujumbe wake kwa mnasaba huo, Mistura ameelezea matumaini yake kwamba mnasaba huu utawawezesha Waislamu na makundi yote ya Iraq kuimarisha umoja kati yao kwa lengo la kufikia amani na utulivu wa kudumu na vilevile kuleta demokrasia katika nchi hiyo ya Kiarabu na Kiislamu. Amesisitiza katika ujumbe wake huo kwamba, Umoja wa Mataifa ungali una azma ya kutekeleza ahadi zake kwa Iraq kuhusiana na kuwasaidia wananchi na serikali ya nchi hiyo kutatua matatizo yao.
Jalal Talabani na Nuri al-Maliki, Rais na Waziri Mkuu wa Iraq kwa utaratibu, pia wamewatumia Waislamu ujumbe tofauti wakiwapongeza kwa mnasaba wa kuwadia sikukuu ya Idul Adh’ha. 331478