IQNA

Ulimwengu wa kweli wa Kiislamu usiokuwa bayana wazinduliwa

12:32 - December 11, 2008
Habari ID: 1717948
Nakala ya majaribio ya ulimwengu wa kwanza wa Kiislamu wa Intaneti usio bayana (virtual world) ujulikanao kama Muxlim Pal imezinduliwa na shirika moja la Uholanzi.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mkuu wa shirika la Muxlim Pal Muhamad El-Fatatry amesema mradi huo wa intaneti utakuwa wa lugha ya Kiingereza na umeanzishwa kwa ajili ya Waislamu hasa waishio katika nchi za Magharibi ambao wanataka kuanzisha uhusiano na Waislamu wa nchi nyinginezo duniani.
Ameongeza kuwa, kwa mujibu wa utaratibu wa mtandao huo, wanaoingia katika ulimwengu huo wa Kiislamu wa "virtual world" wanaweza kujibunia shakhsia, kuchagua mavazi, kujenga nyumba, kuanzisha uhusiano na wengine na kwenda Msikitini kuswali.
Tafauti ya mtandao huu wa intaneti na mitandao yenye huduma kama hizo ni kuwa unazingatia thamani za juu za Kiislamu mbali na kupinga vintendo vya fujo, kuwavunjia heshima wengine na mienendo inayokiuka maadili mema. 332187

captcha