Idara ya Masuala ya Kimataifa ya Jumuiya za Kiislamu za Wanafunzi wa Iran imesema: Suhula zote za mawasiliano zinatumiwa kuwashajiisha wanafunzi wote wa Iran kufikisha ujumbe wa kilio cha watoto wa Gaza kwa walimwengu.
Kila mwanafunzi wa Iran anahimizwa kuandika maeneno mafupi saba kwa lugha bora na yenye taathira kubwa zaidi katika kuunga mkono watu wasio na hatia wa Gaza na kulaani jinai za Wazyuni katika ardhi hiyo ya Wapalestina.
Baadaye mwanafunzi alieyandika ujumbe bora zaidi atatunukiwa zawadi na Muungano wa Jumuiya za Kiislamu Iran. 333495