IQNA

Masoko yafungwa Iran kulaani jinai za Wazayuni Gaza

18:38 - December 15, 2008
Habari ID: 1719542
Wafanya biashara katika maeneo mbalimbali ya Iran wamefunga kazi zao kwa siku moja kama njia ya kulalamikia vikali jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wasio na hatia katika Ukanda wa Gaza na al-Khalil.
Katika maandamano yao ya Jumatatu, wafanya biashara wa Tehran wamelaani jinai za Wazayuni huko Gaza na kutaka kuondolewa mzingiro wa eneo hilo. Huku wakitoa nara kama "Mauti kwa Marekani","Mauti kwa Israel" na "Kumuunga mkono Haniyah ni kuunga mkono Uislamu" waandamanaji hao wametangaza uungaji mkono wao kamili kwa Wapalestina wanaokandamizwa na Wazayuni hasa huko Gaza. Vituo vyote vya biashara ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran vimefungwa Jumatatu kwa masaa mawili kulaani jinai zisizo na kikomo za Wazayuni.
Katika mji mtakatifu wa Qum, masoko pia yalifungwa na wafanya biashara kukusanyika katika msikiti wa soko kuu mjini humo.
Wanachuo wa kidini katika Chuo Kikuu cha Jamiatul Mustafa Al Alamiyya huko Qum pia walisitisha masomo yao kama njia ya kuwaunga mkono Wapalestina na kulaani jinai za Wazayuni. Aidha wamelaani vikali uungaji mkono wa Marekani na nchi za Ulaya kwa utawala katili wa Israel.
Akiwahutubia wanachuo hao, Ayatullah Moqtadai amesifu wanamapambano wanawake na watoto wa Palestina ambao wamesimama kidete kukabiliana na Wazayuni makatili. Ayatullah Moqtadai ametoa wito kwa wanazuoni wa Kiislamu kuchukua hatua za kuwasaidia Wapalestina wanaokabiliwa na masaibu. 334338

captcha