IQNA

Makelele zaidi yapigwe kuwaamsha waliolala kuhusu hali ya kusikitisha Ukanda wa Gaza

17:23 - December 16, 2008
Habari ID: 1719968
Ayatullah Makarim Shirazi ambaye ni mmoja wa wanazuoni wakubwa katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran amesema kuwa makelele zaidi yanapaswa kupigwa kuhusu hali mbaya ya Ukanda wa Gaza huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu ili kuwaamsha Waislamu waliolala.
Ayatullah Shirazi amesema kuwa, dunia ya leo inatawaliwa na migogoro mitatu ya kiuchumi, kimaadili na kiusalama na akaongeza kuwa, inasikitisha kwamba mgogoro wa kimaadili umeenea dunia nzima kupitia vyombo vya mawasiliano ya umma. Kiongozi huyo wa ngazi za juu wa kidini nchini Iran amesema kuwa mabeberu wanafanya dhulma na uonevu wa waziwazi na kwamba mfano wa wazi wa dhulma hiyo unaonekana katika Ukanda wa Gaza. Amesisitiza juu ya kuchukuliwa hatua za kujibu dhulma hiyo na kufichua udhaifu wa madhalimu hao Wazayuni.
Ayatullah Makarim Shirazi amesema: Kelele zaidi zinapaswa kupigwa kuhusu hali mbaya ya raia wa Ukanda wa Gaza ili kuwazindua Waislamu waliolala.
Wakazi milioni moja na nusu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina wanaishi katika mashaka makubwa ya kutokana na mzingiro wa Ukanda wa Gaza. 334110

captcha