IQNA

Wilders na makundi yenye misimamo mikali ya Wazayuni watiliana saini mkataba dhidi ya Uislamu

12:02 - December 21, 2008
Habari ID: 1720989
Kiongozi mwenye misimamo ya kufurutu mipaka wa chama cha Uhuru cha Uholanzi Geert Wilders na taasisi zenye misimamo mikali za utawala wa Kizayuni wa Israel wametiliana saini mkataba wa kuupiga vita Uislamu na hivyo kufichua sura yake ya kifashisti na kupenda kutumia mabavu.
Geert Wilders alishiriki katika kongamano lililofanyika Baitul Muqaddas huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu na Israel ambako alitia saini mkataba wa kuupiga vita Uislamu na Waislamu na kutoa matamshi yasiyokuwa na maana kwa kusema: Mayahudi na Wakristo wanapaswa kuungana kwa ajili ya kupambana na Uislamu na Waislamu. Ameendelea kutoa matamshi yake ya kifashisti kwa kusema: Dini za Kiyahudi na Kikristo ni bora zaidi kuliko Uislamu na kwamba anachele siku ambayo watoto katika nchi za Magharibi watakuwa na kukuta Uislamu umeenea kote barani Ulaya. Mbunge huyo mwenye misimamo ya kufurutu mipaka amedhihirisha sura yaka ya Kizayuni kwa kusema kuwa anaipenda Israel na kwamba utawala huo wa Kizayuni ndiyo serikali pekee ya kidemokrasia katika Mashariki ya Kati!
Geert Wilders ameutaja utawala ghasibu wa Israel kuwa wa kidemokrasia wakati unaendelea kuwaua wanawake na watoto wasiokuwa na hatia wa Kipalestina tena katika ardhi zao na nembo pekee ya demokrasia ya utawala huo ni maafa yanayoendelea sasa katika Ukanda wa Gaza.
Geert Wilders ndiye aliyetengeneza filamu chafu ya Fitna inayovunjia heshima Qur’ani Tukufu. 335692
Kimataifa
captcha