IQNA

Hitilafu za makundi ya Kipalestina, chanzo cha kurefuka mzingiro wa Ghaza

12:12 - December 24, 2008
Habari ID: 1722168
Mufti wa mji wa Quds Sheikh Muhammad Hussein ambaye pia ni khatibu wa msikiti wa Al Aqsa amesema: Ufa na hitilafu zilizopo baina ya makundi ya Kipalestina ndio chanzo kikuu cha kurefuka mzingiro wa Ghaza.
Kwa mujibu wa mtandao wa Intaneti wa Ma’a, Sheikh Muhammad Hussein ametoa taarifa tarehe 23 Disemba akisema: “Hitilafu na ufa miongoni mwa mirengo na makundi ya Kipalestina unahudumia maslahi ya madola ya kibeberu duniani na utawala ghasibu wa Kizayuni. Jambo hilo linauandalia utawala wa Kizayuni wa Israel mazingira ya kuyavunjia heshima maeneo matakatifu ya Kiislamu huko Palestina”.
Sheikh Muhammad Hussein ameongeza kuwa, Quds na matukufu mengine ya Kiislamu yako katika hatari kubwa na kuonya kuhusu mpango wa chuki wa Israel wa Kuiyahudisha Quds Tukufu kwa lengo la kufuta utambulisho wa Kiislamu mjini humo.
Mwishoni mwa taarifa yake Mufti wa Quds ameashiria matatizo ya Wapalestina na kusema, ‘Wapalestina hawana budi ila kufanya mazungumzo, kuimarisha umoja wa kitaifa na Kiislamu na kutokubali wakaazi wa Ghaza wanedelee kuishi katika mzingiro wa Wazayuni’. 337486
captcha