IQNA

11:49 - January 04, 2009
Habari ID: 1726888

Kuundwa kamati ya Ufaransa ya kukabiliana na maslahi ya Israel ulimwenguni

Kufuatia mashambulio ya kinyama ya utawala haramu wa Israel huko katika Ukanda wa Gaza, kamati moja ya shakhsia huru wa Ufaransa wanaotetea haki za binadamu imebuniwa na kuanza kufanya mipango ya kuchunguza njia za kuanzisha harakati za kukabiliana na maslahi ya kiuchumi ya utawaha huo haramu kote duniani.

Chombo kimoja cha habari nchini humo kimesema kuwa, kufuatia kuongezeka kila siku duniani wasiwasi unaohusiana na jinai za kinyama zinazotekelezwa na Israel katika ardhi za Wapalestina na hasa dhidi ya wakazi wasio na ulinzi wala hatia wa Ukanda wa Gaza, kamati hiyo ambayo itawajumuisha pia shakhsia kutoka mataifa mbalimbali imebuniwa na tayari inachunguza njia za kukabiliana na maslahi ya kiuchumi na kibiashara ya utawala haramu wa Israel katika pembe mbalimbali za dunia. Chombo hicho kimesema kuwa kamati hiyo ambayo kimsingi imebuniwa na watetezi wa haki za binadamu wa Ufaransa itatoa mwito kwa jumuiya, mashirika na taasisi mbalimbali za kimataifa kushirikiana nayo katika kufikia lengo hilo. Kamati hiyo imebuniwa katika hali ambayo pendekezo lililotolewa na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa kuhusiana na umuhimu wa Israel kusimamisha mashambulio yake hayo ya kinyama katika kipindi cha masaa 24 kwa ajili ya kuandaliwa mazingira ya kufanyika mazungumzo ya pande mbili hasimu katika mgogoro wa Palestina lilikataliwa na watawala wa utawala huo wa Kizayuni. 810675
captcha