Msemaji wa Bunge la Uturuki amewapelekea barua wenzake katika kamati andamizi ya muungano huo wa mabunge akiwafahamisha juu ya mipango ya kufanyika kikao hicho cha dharura.
Kikao hicho ambacho kitahudhuriwa na Spika wa muungano huo kitajadili mashambulio ya utawala haramu wa Israel na mauaji ya umati yanayotekelezwa na utawala huo dhidi ya watu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza.
Kamati Andamizi ya Muungano wa Mabungu ya Kiislamu ina wanachama 50 zikiwemo nchi za Uturuki, Nigeria, Misri, Mali, Azerbajan, Iran, Algeria, Saudi Arabia, Chad na Benin. 343555