IQNA

9:37 - January 12, 2009
Habari ID: 1729596

Vyombo vya habari vya Kiarabu viakisi jinai za Israel huko Gaza

Ayad Amin Madani, Waziri wa Utamaduni na Habari wa Saudi Arabia amevitaka vyombo vya habari vya nchi za Kiarabu kuuakisia ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu jinai zinazotekelezwa na Israel dhidi ya watu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza.

Akizungumza katika kikao cha 28 cha Baraza Kuu la Muungano wa Redio za Nchi za Kiarabu huko Saudi Arabia, waziri huyo amesema kuwa hujuma ya kinyama inayotekelezwa na Wazayuni huko Gaza pamoja na kuzingirwa ukanda huo ni jinai kubwa dhidi ya jamii ya mwanadamu, jinai ambazo amesema, zinapasa kuakisiwa na vyombo vya habari vya Kiarabu. Amesisitiza kuwa utawala haramu wa Israel unatumia silaha zilizoharamishwa dhidi ya watu wasio na hatia na pia kuzuia misaada ya kibinadamu kuingia katika Ukanda wa Gaza.
Waziri Madani amebainisha matumaini yake kwamba washiriki wa kikao hicho watashinikiza kuondolewa marufuku ambayo inatekelezwa na utawala wa Israel dhidi ya waandishi habari na kuwazuia kuingia katika Ukanda wa Gaza ili kwa njia hiyo waweze kuuakisia ulimwengu jinai kubwa zinazotekelezwa na Wazayuni katika ukanda huo.
Vilevile ametaka vyombo vya habari kuushinikiza utawala huo usimamishe mara moja mauaji ya umati dhidi ya wakazi wa Gaza na pia kusimamisha siasa zake za kuchuja habari zinazotoka katika ukanda huo kuhusiana na jinai unazotekeleza dhidi ya raia wasio na ulinzi. 346457
captcha