IQNA

12:08 - January 17, 2009
Habari ID: 1731648

Hatua ya Venezuela ya kukata uhusianao na Israel imewaaibisha Waarabu

Hatua ya nchi ya Latin Amerika,Venezuela, ya kumfukuza nchini humo balozi wa utawala haramu wa Israel pamoja na kukata uhusiano wake wote wa kisiasa na kibiashara na utawala huo, imewaaibisha watawala wote wa Kiarabu wanaoshirikiana na kufanya mapatano na utawala huo.

Hayo yamesemwa na Ayatullah Qassim at-Tai, maraja' na mwanazuoni mashuhuri wa Iraq. Mwanazuoni huyo ametoa taarifa katika mji mtakataifu wa Najaf akisema kwamba, hatua ya kishujaa iliyochukuliwa na Rais Hugo Chaves wa Venezuela imekaribishwa na kupokelewa kwa moyo mkunjufu na umma mzima wa Kiislamu.
Ayatullah at Tai amesema kuwa utawala haramu wa Israel ni tishio kubwa kwa usalama na amani ulimwenguni na kuongeza kuwa watu wasio na hatia wa Gaza na hasa watoto na wanawake wamekuwa wahanga wa dhulma ya taasisi za kimataifa.
Mwishoni mwa taarifa hiyo, Ayatullah at-Tai ameshangazwa na misimamo ya baadhi ya watawala wa nchi za Kiarabu na kusisitiza kwamba bila shaka vita vya Gaza ni hujuma ya moja kwa moja ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Waislamu. 349106
captcha