IQNA

Misri yazuia ujumbe wa Kiislamu wa Ulaya kuingia Gaza

16:18 - January 17, 2009
Habari ID: 1732060
Viongozi wa Misri wameuzuia ujumbe wa Kiislamu wa Ulaya kuingia katika Ukanda wa Gaza kupitia kituo cha mpakani cha Rafah.
Duru za habari zimeripoti kuwa ujumbe huo wa Kiislamu wa Ulaya unaojumuisha wanasheria na madaktari wa Kiislamu kutoka nchi za bara hilo ulikusudia kuelekea Ukanda wa Gaza kupitia kivuko cha Rafah lakini ulizuiwa na maafisa wa serikali ya Misri.
Shakib bin Makhluf, Mwenyekiti wa Muungano wa Jumuiya za Kiislamu nchini Ufaransa amesema kuwa misaada ya kibinadamu ya ujumbe huo inayojumuisha madawa na zana za kitiba ilivuka mpaka jana na kupelekwa Gaza lakini viongozi wa Misri wameuzuia ujumbe huo kuingia katika eneo hilo.
Shekib Makhluf amesema: Muungano wa Jumuiya za Kiislamu barani Ulaya inalaani vikali jinai za Israel katika Ukanda Gaza na inafanya juhudi kubwa za kusimamisha mauaji ya kizazi ya utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi wa eneo hilo. Ameongeza kuwa kwa sasa muungano huo unafanya juhudi za kuwafungulia mashtaka viongozi wa Israel katika mahakama ya kimataifa. 349425
captcha