IQNA

Yemen yafungua kituo cha kwanza cha kijeshi kwa wanaojitolea kupigana huko Gaza.

10:52 - January 19, 2009
Habari ID: 1732754
Yemen imefungua kituo cha kwanza cha watu wanaojitolea kwenda katika Ukanda wa Gaza kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zao wanaokandamizwa na kuuawa kwa umati na majeshi ya utawala haramu wa Israel.
Kituo hicho ambacho kimefunguliwa kwa ushirikiano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar, kiko katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Imani mjini Sanaa.
Sheikh Abdul Majid Zandani, Mkuu wa Chuo Kikuu hicho ndiye aliyepewa jukumu la kusimamia kituo hicho. Sheikh Zandani amesema kuwa watu watakaojitolea kupigana bega kwa bega na ndugu zao Waislamu huko katika Ukanda wa Gaza watakuwa wakipewa mafunzo katika kituo hicho. Ametaka watu kujitolea na kujiandikisha katika kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia ndugu zao wa Hamas dhidi ya mashambulio ya kinyama ya Wazayuni.
Marekani imemuweka Sheik Zandani katika orodha ya watu wanaotuhumiwa nanchi hiyo kuwa magaidi kwa madai kwamba anaisaidia kifedha Hamas, lakini viongozi wa Yemen wametupilia mbali tuhuma hizo wakisema kuwa iwapo dalili za kutosha zitapatikana dhidi ya kiongozi huyo, basi watalazimika kumuhukumu wenyewe ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
Wakati huohuo, Rais Ali Abdallah Swaleh wa Yemen amezitaka nchi za Kiislamu kuwafungulia mlango wa jihadi watu wanaojitolewa kwa ajili ya kwenda kupambana bega kwa bega na ndugu zao wa Gaza dhidi ya wavamizi na watenda-jinai wa Kizayuni. 350251
captcha