IQNA

Tukio la Ashura linatoa sura ya kipekee ya Mashia duniani

16:02 - January 24, 2009
Habari ID: 1735192
Hakuna shaka kuwa maombolezo makubwa duniani ni yale ambayo hufanyika katika kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein AS na hili limewafanya Waislamu wa Kishia kuwa na sura ya kipekee mingoni mwa madhehebu na dini zote duniani.
Hujjatul Islam Walmuslimin Mahmoud Taqizade Davari ameyasema hayo katika kongamano la Utambulisho wa Kijamii na Kisiasa wa Mashia lililofanyika tarehe 22 Januari katika mji mtakatifu wa Mash'had, Iran. Amesema kuwa katika vikao vya maombolezo ya siku ya Ashura, mbali na thawabu za kidini zinazopatikana, maombolezo hayo pia yana nukta muhimu kwa jamii ya Mashia. Mojawapo wa faida hizo ni kuwa maombolezo hayo huwa chanzo cha kuimarisha umoja miongoni mwa Waislamu wa Kishia kwani wote hushiriki kwa raghba katika halfa hizo.
Amesema, vikao vya kuomboleza kuuawa Shahidi Imam Hussein AS na wafuasi wake watiifu ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za kuendeleza suna za jadi kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Akizungumza katika kongamano hilo, Hujjatul Islam wal Muslimin Muhsin Alviri wa Chuo Kikuu cha Imam Sadeq AS amezungumzia kuhusu suala la Ashura na Utamaduni wa Kishia na kusema: "Tukio la Ashura limeathiri sekta zote za maisha ya Mashia". 352794

captcha