Kwa mujibu wa Shirka Rasmi la Habari la Kuwait KUNA, wasomi na wahuburi kadhaa wa Kiislamu nchini Sweden pamoja na maulamaa kutoka nchi kadhaa za uliwemwengu wa Kiislamu wameshiriki katika kongamano hilo.
Washiriki wa kimataifa walikuwa ni pamoja na Sheikh Uthman Khamis na Sheikh Faisal Fazar ambao ni maulmaa kutoka Kuwait, Ahmad Al Kous Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Misaada ya Masomo ya Quran na Suna ya Kuwait, Abdallah Al Junaidi Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ansar Sunna al Muhamadiyya ya Misri na Ahmad Al Kus Rais wa Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Senegal.
Katika kongamano hilo, wazungumzaji walijadili maudhui kama vile, "Njia za Kutetea Sira na Suna ya Mtume SAW", "Kubainisha Utukufu, Karama na Maadili ya Mtume SAW" na " Jibu kwa hujuma na matusi ya baadhi walio na chuki wanaotoa taswira za kumvunjia heshima Mtume SAW.
Idadi kubwa ya Waislamu ambao ni wachache nchini Sweden walishiriki pia katika kongamano la kimataifa la kumtetea Mtume (saw). Walichunguza hali na matatizo ya Waislamu wa Sweden, kuimarisha zaidi mshikamno wa Waislamu na Qur'ani Tukufu na Suna ya Mtume SAW na vile vile kuwaita Waislamu na wasio kuwa Waislamu katika meza ya mazungumzo na kuishi pamoja kwa amani na kuheshimiana. 353454