Taarifa iliyotolewa na Jumuiya ya Kiislamu ya Amani Duniani imesema, mtandao huo pia utakuwa na makala zenye maudhui kuhusu amani na ugaidi.
Jumuiya ya Kiislamu ya Amani Duniani ni taasisi isiyo ya kiserikali na itafanya kazi kwa kuzingatia misingi na thamani amani, uadilifu na kwa kutegemea thamani za kibinaadamu, dini, maadili na utamaduni wa mwanadamu.
Jumuiya hiyo inasisitiza juu ya udharura wa maelewano ya wanadamu, ufungamano wa dini, staarabu na tamaduni mbalimbali duniani.
Aidha jumuiya hiyo inakusudia kubainisha mabalaa ya vita na ukosefu wa amani na kuhimiza mazunguzmo kwa msingi wa falsafa ya mantiki na akili.
Mtandao huo utazindua sehemu yake ya lugha ya Kiingereza katika siku zijazo.
Anwani ya mtandao huo ni http://www.islamicworldpeace.com
354592