Kikao cha kitaalamu cha wasomaji wakongwe na wale wa kimataifa wa Qur'ani Tukufu kinafanyika hii leo mjini Tehran. Kikao hicho kitahudhuriwa na Ustadh Farajullah Shadhili, Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wasomaji wa Qur'ani ya Misri.
Mshauri wa Idara ya Mawasiliano ya Baraza Kuu la Qur'ani nchini Iran amesema kuwa kikao hicho cha mafunzo na utafiti cha walimu na wasomaji hodari wa Qur'ani nchini Iran kitaanza kazi zake leo katika Husainiya ya al Zahra mjini Tehran na kuchunguza masuala ya kiufundi ya usomaji Qur'ani.
Warsha ya kiraa ya Qur'ani kwa ajili ya wasomaji vijana itaanza kesho Alkhamisi. Kikao hicho kitahudhuriwa pia na Ustadh Farajullah ambaye atachunguza na kuchambua kiraa za wasomaji vijana wa Kiirani.
Ni vyema kukumbusha hapa kuwa Baraza Kuu la Qur’ani nchini Iran kila mwaka huitisha vikao vya kitaalamu vinavyowashirikisha walimu na maustadhi bingwa wa Qur’ani kutoka Misri kwa ajili ya kustawisha kiwango na vipawa vya wasomaji Qur’ani vijana nchini Iran. 354936