IQNA

13:52 - February 03, 2009
Habari ID: 1739557

Kukurubishwa pamoja madhehebu za Kiislamu, matunda makubwa zaidi ya Mapinduzi ya Kiislamu

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni mapinduzi yaliyokuwa ya kiungu, yanayoungwa mkono na wananchi, yanayotetea wanyonge na kupinga madhalimu. Matunda makubwa zaidi ya mapinduzi hayo ni kuhuishwa moyo na harakati za kukurubisha pamoja madhehebu za Kiislamu kote ulimwenguni.

Hayo yamesemwa na Muhammad Mahdi Ahmadi, Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran chini Qatar. Amesema, mtazamo wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran wa kuletwa umoja kati ya madhehebu ya Shia na Sunni ulitekelezwa kivitendo na kupokelewa kwa mikono miwili katika ulimwengu wa Kiislamu na wanafikra pamoja na wasomi muhimu wa Kiislamu, wasomi ambao wenyewe wamekuwa katika mstari wa mbele wa kudumisha fikra na mtazamo huo.
Huku akiashiria masuala yaliyopelekea kupatikana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, Bwana Ahmadi amesema kuwa azma na imani ya kidini pamoja na itikadi ya taifa la Iran, uungaji mkono mkubwa wa wananchi kwa viongozi wa Mapinduzi na kuwepo kwao katika medani ya mapambano ni miongoni mwa mambo ambayo yalikuwa na nafasi muhimu katika ushindi wa mapinduzi hayo.
Ahmadi amesema kuwa, kulindwa kwa masuala hayo na hasa kuzingatiwa tabaka la vijana katika uendeshaji wa masuala ya mfumo wa Kiislamu ni jambo muhimu katika kudhamini mustakbali wa mfumo huu.
Shakhsia huyo wa masuala ya kiutamaduni amesema, anaamini kwamba kuheshimiwa matakwa ya wananchi na kufahamishwa kwao matunda muhimu ya Mapinduzi ya Kiislamu ni suala muhimu na lenye athari kubwa katika kuimarisha mfungamano wa serikali na wananchi na hivyo kudhihirisha nguvu ya Mapinduzi ya Kiislamu katika upeo wa kimataifa.
Bwana Ahmadi amesema kuwa, kwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, fikra mpya ya uongozi wa Kiislamu iliweza kudhihiri ulimwenguni, na kuchukua nafasi muhimu katika kukabiliana na ubepari wa Magharibi na Ukomunisti wa Muungano wa Sovieti ya zamani. Amesema, fikra za Imam Khomeini (MA), mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, kama vile uadilifu, utukufu wa mwanadamu, utukufu wa Waislamu, mapambano dhidi ya dhulma ni jambo lililofanya fikra hizo za Mapinduzi ya Kiislamu ambazo zinaoana kikamilifu na maumbile ya mwanadamu, kuweza kuenea kwa haraka ulimwenguni.
357695
captcha