IQNA

11:27 - February 05, 2009
Habari ID: 1740475

Kituo cha kwanza cha mafunzo kwa wahubiri wa Kiislamu chafunguliwa nchini Brazil

Kituo cha kwanza cha mafunzo kwa ajili ya wahubiri wa Kiislamu katika nchi za Latin Amerika kitafunguliwa nchini Brazil. Abdul Baqi Othman, mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kiislamu cha Latin Amerika amesema kuwa kituo hicho kitafunguliwa Jumapili tarehe Mosi mwezi ujao wa Machi.

Ameongeza kuwa lengo lake kuu litakuwa ni kutoa mafunzo kwa wahubiri na mahatibu wa Kiislamu. Bwana Othman amesema kuwa, Waislamu wa eneo la Latin Amerika wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa wahubiri wa Kiislamu na kwamba wahubiri wa Kiislamu ambao hivi sasa wanajishughulisha katika eneo hilo wanatoka katika nchi za Kiislamu na Kiarabu. Amesema, kutojua kwao lugha ya wenyeji wa eneo hilo ni kikwazo kikubwa katika utekelezaji wa majukumu yao.
Abdul Baqi Othman ameendelea kusema kuwa, katika hali ya hivi sasa kuna vituo vya Kiislamu, misikiti na maeneo ya ibada na mafunzo ya Kiislamu yapatayo 1200 nchini Brazil ambayo yanakabiliwa na uhaba mkubwa wa wahubiri na walimu wa Kiislamu.
Kuhusiana na suala hilo, Muhsin bin Musa al-Husseini, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislamu ya jimbo la Barana nchini Brazil amesema kuwa Waislamu wa nchi hiyo wamelazimika kuanzisha kituo hicho cha mafunzo kwa wahubiri wa Kiislamu kutokana na nchi za Kiislamu na Kiarabu kutokuwa tayari kutuma wahubiri wa kutosha katika nchi hiyo hiyo. Amesisitiza kwamba, tatizo hilo haliihusu Brazil tu bali nchi zote za Latin Amerika. 359261
captcha