IQNA

11:13 - February 05, 2009
Habari ID: 1740480

Russia kutayarisha mkutano wa kimataifa wa kuikarabati Gaza

Mwakilishi wa kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa Vitaly Chorkin amesema kuwa nchi hiyo itatayarisha mkutano wa kimataifa wa kulikarabati eneo la Ukanda wa Gaza.

Kituo cha habari cha Russia Today kimeripoti kuwa Vitaly Churkin amesema, mkutano huo utahudhuriwa na wanasiasa maarufu kutoka pembe mbalimbali za dunia na kwamba utafanyika baada ya mkutano mwingie kama huo wa Cairo, Misri.
Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema, Moscow itadumisha ushirikiano wa kimataifa kwa ajili ya kutafuta suluhisho la changamoto na matatizo mbalimbali ya dunia na kwamba mkutano wa kimataifa wa kuikarabati Gaza ni katika mikakati ya Russia ya kutaka kurejesha amani katika eneo la Mashariki ya Kati.
Vilevile ameutaka utawala wa Kizayuni wa Israel kufungua vituo vyote vya mpakani vya Gaza kwa ajili ya kuingiza misaada ya kibinadamu katika eneo hilo na kuheshimu maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yanayosisitiza juu ya udharura wa kulinda haki za raia. 359439

captcha