Zaidi ya wanafikra 200 wakiwemo wasomi na wataalamu wa masuala ya habari kutoka ulimwengu mzima wa Kiisalmu wanahudhuria mkutano huo. Wanajadili masuala mbalimbali yanayohusiana na vyombo vya habari vya kisasa na namna vinavyotumiwa kutusi itikadi na nembo za kidini.
Akihutubia katika ufunguzi wa kongamano hilo, Hassan Ahmad Alwazi, Waziri wa Habari wa Yemen amesema, kikao hicho kitajadili kuhusu 'vita vya Msalaba na athari zake za kihistoria katika kuchafua taswira ya Uislamu', 'taswira ya Uislamu na Waisalmu katika mfumo wa elimu wa nchi za Magharibi' na 'changamoto za kisiasa na kiuchumi katika Ulimwengu wa Kiislamu na athari zake katika kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiisalmu'.
Kongamno hilo pia linahudhuriwa na Abdullah Bin Abdulmuhsin Al Turki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ulimwengu wa Kiislamu . 360475