IQNA

15:04 - August 21, 2026
Habari ID: 3482655

Qari wa Misri afaulu katika taaluma ya tiba na usomaji wa Qur’ani

IQNA – Salah al-Jamal ni daktari kutoka Misri ambaye amepata mafanikio makubwa katika nyanja za kuhifadhi na kusoma Qur’ani Tukufu.

Qari wa Misri afaulu katika taaluma ya tiba na usomaji wa Qur’aniKatika mahojiano na Nafi’ Al-Taras, kwenye kipindi cha “Mwananchi na Afisa” kinachorushwa na televisheni ya satelaiti ya Shams, al-Jamal alielezea safari yake ya Qur’ani, kutoka kijiji cha Aweesh Al-Hajar, katika mkoa wa Dakahlia nchini Misri, hadi kufikia umaarufu wa kimataifa.

Alisisitiza kwamba kuhifadhi Qur’ani akiwa katika umri mdogo kulikuwa hatua ya mabadiliko makubwa katika maisha yake. Alisema baraka alizoandamana nazo katika njia hiyo zimemsaidia kuunganisha masomo yake ya udaktari na huduma kwa Kitabu Kitukufu cha Allah.

Al-Jamal alisema kuwa alihifadhi Qur’ani yote katika kijiji chake akiwa na umri wa miaka 10, na akiwa na miaka 11 alipata nafasi ya pili katika mashindano ya kitaifa ya Qur’ani.

Alifafanua kwamba hatua kuu ya mabadiliko katika maisha yake ilitokea mwaka 1995, alipokwenda Afrika Kusini kuswalisha katika nyakati za usiku za Ramadhani. Huko, bila kutarajia, alijikuta akishiriki mashindano ya kimataifa ya usomaji wa Qur’ani, ambako alishinda nafasi ya kwanza.

Qari huyo wa Misri alisema tukio hilo lenye heri lilimfungulia milango mipya: alianza kusafiri mara kwa mara nje ya nchi kuhuisha nyusiku za Ramadhani, huku jina lake likihusishwa na matangazo ya moja kwa moja kupitia Idhaa ya Qur’ani.

Aliongeza kuwa serikali ya Misri ilimtunuku heshima baada ya kurejea nchini, na ikamfungulia milango ya Idhaa ya Qur'ani. Aliweza kufanya mitihani ya redio na kufaulu kwa jaribio la kwanza. Baadaye, kamati ya redio ilimpatia mafunzo kuhusu stadi za usomaji wa Qur’ani, na ndipo shughuli zake za redio katika kuitumikia Kitabu cha Allah zikaanza.

Al-Jamal alisisitiza kuwa taaluma yake ya udaktari haikugongana na safari yake ya Qur’ani. Alijiunga na Kitivo cha Tiba mjini Cairo, na baada ya miaka saba alihitimu na kubobea katika upasuaji wa jumla. Baadaye alifungua kliniki yake binafsi katika eneo la Imbaba, Cairo.

Qari huyo alisema kuwa kujishughulisha kwake na tiba na kazi hakukukata uhusiano wake na Qur’ani. Alieleza kuwa anajiona kuwa mpenzi na mhudumu wa Qur’ani, si msomaji wa kitaaluma kwa maana ya kibiashara. Licha ya masomo na majukumu yake ya kazi, anadumu kusoma Qur’ani kila siku.

Akizungumzia ratiba yake ya kila siku ya kuoanisha taaluma ya tiba na Qur’ani, al-Jamal alisema hutenga saa za usiku kwa ajili ya ibada kulingana na uwezo na mazingira yake, na husoma juzuu tatu hadi nne za Qur’ani kila siku.

Alisisitiza kwamba mtindo huo wa maisha unaonesha kuwa inawezekana kufanikiwa katika nyanja zaidi ya moja, iwapo mtu atadumisha lengo lake na kutumia muda wake kwa namna bora.

Aliongeza kuwa Qur’ani imekuwepo katika maisha yake sambamba na elimu yake ya tiba, taaluma yake, na kazi zake za redio.

Ifuatayo ni video ya Salah al-Jamal akisoma Qur’ani Tukufu.

3498720

Habari zinazohusiana
captcha