Kwa mujibu wa mwandishi wetu mjini Beirut, katika mkutano huo uliofanyika katika kasri ya rais, Balozi Sheibani alitoa ufafanuzi juu ya uchunguzi unaoendelea kuhusu wanadiplomasia hao wanne Wairani waliotekwa nyara na kutoweka mwaka 1982.
Sheibani amesema kuwa Utawala ghasibu wa Israel ndio unaobeba lawama ya kutoweka wanadiplomasia hayo.
Rais Michel Suleiman amesema wanadiplomasia hao Wairani walitoweka katika vita vya Lebanon. Amesema, anashauriana na wataalamu na mawaziri ili hatima ya wanadiplomasia hao wa Iran iweze kuwekwa wazi. ‘Nawatala maafisa husika kuongeza jitihada zao katika kupata taarifa zaidi kuhusu hatima ya wanadiplomasia hawa’, amesema Rais Suleiman.
Ahmad Mutawasilian, Muhsen Musawi, Kadhim AKhawan na Ahmad Rastgar Muqaddam ni wanadiplomasia wanne wa Iran ambao walitekwa nyara na kutoweka Lebanon mwaka 1982. Wanadiplomasia hao walitekwa nyara na wanamgambo wa Kikristo wa Phalanga ambao ni waitifaki wa utawala wa Kizayuni wa Israel. 361300