IQNA

12:06 - February 10, 2009
Habari ID: 1742335

Kuandikwa aya za Qur’ani katika relitheluji kwawakasirisha Waislamu wa Kashmir

Kuwepo aya za Qur’ani Tukufu katika relitheluji za mtalii mmoja wa Sweden ambaye alikuwa ameenda kucheza mchezo wa kuteleza kwenye theluji yaani skii katika eneo la Gulmarg huko Kashmir kumeamsha hasira kubwa ya Waslamu wa eneo hilo

Tovuti ya KashmirWatch imeandika kuwa, mara tu baada ya kuenea habari hiyo, Waislamu wa Kashmir walikusanyika katika eneo hilo na kulalamikia vikali jambo hilo.
Baada ya kushuhudia mkusanyiko huo mkubwa wa Waislamu, polisi ilimkamata mtalii huyo mara moja na kumsaili kuhusiana na jambo hilo.
Baada ya mahojiano, mtalii huyo alisema kuwa mkewe ambaye ni raia wa Qatar siku chache zilizopita alimpa vipachiko ambavyo vilikuwa vimeandikwa juu yake aya za Qur’ani Tukufu naye akaamua kuvibandika kwenye relitheluji hizo bila ya kutambua athari na matokeo yake. 361379
captcha