Hayo yamesemwa na Farouq, Abdul Ghani Rizq, Naibu Mkuu wa Jumuiya ya Wasanii wa Kiarabu ambaye ni mgeni wa tamasha ya Filamu ya Fajr nchini Iran. Amesema, filamu za katuni hai, visa kwa watoto na kufahamishwa watoto fadhila za Ahlul Beit (as) kwa ajili ya kueneza Uislamu ni njia bora zaidi zinazoweza kutumika kuhusiana na suala hilo.
Kuhusiana na nafasi ya vyombo vya habari katika kueneza mafundisho ya Uislamu, Bwana Abdul Ghani Rizq amesema kuwa vyombo hivyo vina umuhimu mkubwa na kwamba kila fursa inapasa kutumiwa vyema kwa lengo la kuvitumia vyombo vya habari katika kueneza mafundisho halisi ya Kiislamu ulimwenguni.
Katika upande mwingine, Bibi Najwa Ibrahim Ahmad, mbaye ni mwandishi wa matini za filamu na mtaalamu wa masuala ya filamu na mgeni mwingine wa tamasha ya Filamu ya Fajr amesema kuhusiana na sababu ya nchi za Magharibi kutengeneza filamu za kupotosha na matusi dhidi ya Uislamu kwamba, jambo hilo kimsingi linatokana na kutokuwepo kwa vyombo muhimu na vyenye nguvu vya upashaji habari katika ulimwengu wa Kiislamu, na kwamba nchi za Kiislamu zinapasa kutengeneza filamu zinazotegemea dalili na hoja zenye nguvu kwa ajili ya kukabiliana na filamu hizo za Magharibi zinazolenga kupotosha na kutusi thamani na matukufu ya Kiislamu. 361546