Ismail Pirnia, mkuu wa Kamati ya Utamaduni ya Olimpiadi ya Nne ya Kimataifa ya Qur'ani na Hadithi ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha "Jamiatul Mustafa (SAW) al Alamiya" kilicho katika mji mtakatifu wa Qum nchini Iran amesema kuwa:"Kwa kuzingaitia idadi kubwa ya waliojiandikisha kushiriki katika duru hii ya Olimpiadi, tumeongeza muda hadi Februari 18 ili kutoa fursa kwa wapendao kushiriki kujiandikisha".
Pirnia ameongeza kuwa muhula wa awali wa kujiandikisha ulikuwa unamalizika tarehe 13 Februari lakini baada ya mashauriano na idara ya maandalizi ya Olimpiadi imeafikiwa kuongeza muhula wa kujiandikisha.
Taasisi za kitaifa na kigeni zilizochini ya Chuo Kikuu cha "Jamiatul Mustafa (SAW) al Alamiya" zinaweza kukubali maombi ya wanaotaka kushiriki hadi tarehe 18 Februari. 362730