Gazeti la Saudi Arabia la as-Sharqul Ausat limeandika kuwa, Ihsanoglu amesema katika taarifa kuwa, lengo la makundi hayo ya kigaidi na yenye misimamo ya kupindukia mipaka ni kuzusha mgongano kati ya waomboleza wa Kishia na makundi mengine ya kimadhehebu ya Iraq.
Huku akibainisha masikitiko yake makubwa kuhusiana na tukio hilo, Ihsanoglu amewataka wafuasi wa madhehebu tofauti za Kiislamu nchini Iraq kuimarisha umoja na mshikamano wa Kiislamu miongoni mwao na kufanya juhudi za kuvunja njama za maadui wa Uislamu za kuzusha mfarakano na hitilafu za kimadhehebu miongoni mwa Waislamu wa nchi hiyo.
Mlipuko wa kigaidi uliotokea siku kadhaa zilizopita nchini Iraq umepelekea watu wasiopungua 40 kupoteza maisha yao na wengine 80 kujeruhiwa.
Waislamu hao walikuwa katika msafara uliokuwa ukielekea katika mji wa mtakatifu wa Karbala kuomboleza mauaji ya mjukuu wa Mtume Muhammad (saw) Imam Hussein (as) 364383