IQNA

11:50 - February 18, 2009
Habari ID: 1745474

Benki Kuu ya Ufaransa mwenyeji wa kikao cha 'Huduma za Kifedha za Kiislamu'

Kikao cha tatu cha 'Huduma za Kifedha za Kiislamu' kitaandaliwa na Benki Kuu ya Ufaransa tarehe 4 Machi huko Paris, mji mkuu wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa NOVOpress, kikoa hicho kitafanyika kwa madhumuni ya kuanzisha uhusiano wa kiuchumi baina ya benki za Ufaransa na taasisi za kifedha za nchi za Ghuba ya Uajemi na pia kuenezwa uchumi wa Kiislamu katika nchi za Ulaya.
Kikao hicho kimeandaliwa baada ya Christian Noyer, Mkuu wa Benki Kuu ya Ufaransa na Arnaud de Bresson, mwakilishi wa Taasisi ya Kifedha ya Paris Europlace kufanya safari mjini Bahrain, Qatar, Abu Dhabi na Dubai kwa lengo la kuwasilisha huduma za kisasa za kiuchumi za Ufansa na pia kuvutia uwekezaji wa nchi za Kiislamu.
Mwaka uliopita, Spika wa Seneti ya Ufaransa aliwasilisha makala yenye kichwa kisemacho 'Uchumi wa Kiislamu' ambapo alichunguza nafasi ya uchumi wa kisasa katika kuainisha hatima ya masoko ya dunia na pia athari za uchiumi wa Kiislamu na itibari za benki katika mtazamo wa sheria ya Kiislamu.
Waziri wa Uchumi wa Ufaransa pia alitoa ahadi kwamba serikali ya Paris itafanya juhudi za kuoanisha mifumo ya kiuchumi ya Ufaransa na ya Kiislamu.365226
captcha